Dr. Jakaya Mrisho Kikwete katikati akiwa na Mh. Anna Makinda spika wa bunge la Jamuhuri la muungano wa Tanzania aliyevaa gauni jekundu wakiongozana na Waziri Steven Wasila aliyevaa suti nyeusi pembeni mwa muhushimiwa Anna Makinda kushoto ni Dr. Seiph Iddy makamu wa raisi awamu ya pili kushoto kwake ni mh. Dr. Rehema Nchimbi
Muheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania akiongea na mkurugenzi mkuu wa TASAF katika uzinduzi wa TASAF uwanja wa jamuhuri stadium mjini Dodoma
Dr. Jakaya Kikwete akiangalia baadhi ya bidhaa zinazo tengenezwa na wajasilia mali waliowezeshwa na TASAF,katika uzinduzi wa TASAF mjini Dodoma wajasilia mali hao wanajihusisha na bidhaa mbalimbali kama biashara ya ubuyu,mabatiki pamoja na uchujaji wa mafuta ya ubuyu.
Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr, Jakaya Mrisho kushoto ni Mh.Anna Makinda na kulia ni Dr. Rehema Nchimbi mkuu wa mkoa wa Dodoma wakiangalia baadhi ya makundi ya wacheza ngoma katika sherehe za uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF iliyo fanyika mkoani Dodoma
Kikundi cha wenyeji Dodoma kikitumbuiza katika uzinduzi wa TASAF awamu ya tatu mkoani Dodoma kama unavyo ona pichani
Kikundi abacho kiliimba kwa lugha y kigogo pichani kama kinavyo onekana wakitumbuiza katika uzinduzi huo mkoani Dodoma
Sheheh Ahmed Msuli akifanya maombi katika shughuli hiyo kabla ya raisi wa nchi kuja kuutubia umma
Askofu father Chesco wa Dodoma akifanya maombi katika shughuli hiyo kabla ya raisi wa nchi kuja kuutubia umma
Katikati Dr. Jakaya Mrisho Kikwete upande wake wa kushoto ni makamu raisi awamu ya pili Mh.Seiph Iddy na upande wa kulia ni Mh. Anna Makinda wakiwa wameketi meza kuu katika uzinduzi wa TASAF mkoani Dodoma
Mh.Rehema Nchimbi mkuu wa mkoa wa Dodoma akiwatambulisha wageni rasmi katika uzinduzi wa TASAF mkoani Dodoma
Mdau wa TASAF Mh. Idda Manjoro kutoka Malawi akiongelea mchango wake katika kuinua kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi
Pichani hapo juu ni mwanamuziki wa kizazi kipya Diamond Platinum baada ya CD aliyo kuwa akitumia kugoma kupiga na kama unavyo muona ni mtu mwenye ghazabu sana katika uzinduzi huo wa TASAF
Baadhi ya watu ambao wakisubiri kuchangia damu katika banda la changia damu salama mkoani Dodoma ilifanyika katika uzinduzi huo huo wa TASAF
huu ni mtoto akitoa hushuhuda TASAF ilivyo mtendea mema alikuwa hana sale za shule lakini sasa ni mtu katika watu kwani sale amepata na anaendelea na shule vizuri
Waziri wa nchi ofisi ya raisi sela na mipango Mh. Steven Wasila akimkalibisha Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa ajiri ya kutoa utuba kwa wananchi na kuzindua rasmi awamu ya tatu ya TASAF mpango wa taifa wa kunusuru kaya maskini zilizo katika mazingira hatarishi
Habari na Matukio:Paul Lawa

0 comments:
Post a Comment