Latest Post

Saturday, September 29, 2012

DODOMA ENTERTAIMENT

|0 comments
DODOMA ENTERTAINMENT WANAKULETEA SHOW KABAMBE INAYO HUSISHA VIPAJI MBALIMBALI IKIWEMO WASANII CHINI YA UMRI WA MIAKA KUMI NA NANE ILIYO FANYIKA KATIKA UKUMBI WA CLUB LA AZIZI

Lengo katika shughuli hii ni kuinua vipaji vya watoto (under 18's,vipaji kuimba pamoja na kucheza show hiyo imezaminiwa na Tigo express your self,Dodoma fm radio 98.4,Grey Electronics,Zunny Icecream,Ulanga lodge,pamoja na Dodoma printing.
Katika sherehe hiyo walikuwepo majaji wa kutafuta vipaji vya wasanii chini ya miaka kumi na nane Rabiaman show,Anna Daud,Josephin Kaponya pamoja na maproducer kutoka studio tofauti kutoka dodoma.
Show ya kucheza ilifunguliwa na Juma Madaraka ambaye aliingia na ngoma zetu akifuatiwa na wezake watatu.
Ilifuatiwa na show kabambe kutoka kwa vijana mahili ambao wana uwezo wa kulishambulia jukwaa kwa uwezo usio wa kimfano ambao walivalia nyekundu na nyeusi,bila kukubali kushindwa vijana wa Dodoma fm 98.4 nao waliingia na kuzisakata kwaito za south,haikuishia hapo wana Tigo nao waliamua kuingia maeneo hayo ya uwanja unataka kuona ilikuwaje fungua hapo chini na uangalie full video,unafikili utamu uliisha walizidi kuingia watu wengi si unajua tena kitu cha Zombo tena utata mtupu watu walikisababisha,Haikuishia hapo tigo si walipewa nafasi yao wenyewe wakinukishe dah tigo acheni waitwe tigo walisababisha ile mbaya ni noma fungua tu angalia show ilivyo kuwa ni kazi kubwa ya dodoma entertainment iliyo zaminiwa na dodoma fm 98.4,
show nzima ilikuwa ni kutafuta washindi watatu tu ambao mshindi wakwanza atapewa zawadi na tigo,na dodoma fm 98.4 aliweza kuwapatia zawadi washindi watatu hao kulekodi singo katika studio kubwa na kali hapa dodoma mjini,katika awamu ya pili ilianza na kupatikana washindi kumi na tano wa mwanzo.nusu fainali ilitarajiwa kubakiwa na watu watano tu ili kuweza kupata washindi watatu katika upande wa kuimba na kuchana.
wasanii waliendelea kupunguzwa ili litimie lile lengo la kuwapata washindi watatu tu,kama kawaida wasanii walio bolonga walipewa changamoto mbalimbali kutoka kwa majaji

Monday, September 17, 2012

JE?AJARI BARABARANI ZINASABABISHWA NA NANI MTEMBEA KWA MIGUU AU DEREVA

|0 comments





 DEREVA WA DARADARA AMKOSAKOSA MZEE MMOJA MITAA YA BARABARA YA SABA NA KUZUA BARAA KUBWA
 













 Mzee huyo ambaye alikoswakoswa na gari aina ya daradara na kuzua baraa kubwa baada ya mzee huyo kukasilika na kukaa mbele ya gari hiyo na kuanzisha fukuto katika gari na kusababisha abiria wote walio kuwemo katika gari hiyo kutelemka na kuendeleza timbwili katika mtaa huo wa barabara ya saba mjini dodoma karibu na Diamond Trust Bank,hakuishia hapo mzee huyo aliamua kupiga ngumi kioo cha gari hilo na kumfanya dereva kukasilika na kusababisha msongamano wa magari mengi sana haikuishia hapo,baada ya askari wa barabarani kuwasili ndo ugomvi baina ya mzee huyo na dereva kuisha baada ya mzee huyo kupelekwa kituo kikubwa cha polisi

Saturday, September 15, 2012

ULE MPANGO WA KUSAKALANYA BONGO MOVIE VIPAJI VIPYA KABISA KATIKA TASNIA YA KUIGIZA

|0 comments



































MAANDALIZI YA SERENGETI FIESTA 2012 MJINI DODOMA JINSI YA LIVYO KUWA

|0 comments
 Hawa ni wafanyakazi wa GAPCO ambao ndo walio husika kutengeneza jukwaa ambalo litatumika kwenye fiesta serengeti
Mfanyakazi wa GAPCO akijaribu kuchomeka vyuma vya jukwaa.
Wafanyakazi wa GAPCO wakifunga nati za jukwaa ili kupandisha juu 

wafanyakazi hao wakijaribu kunyanyua nguzo hizo anbazo zimeungwa kwa vyuma