Sunday, August 12, 2012

Habari na Matukio

BAADHI YA WAFANYAKAZI MBALIMBALI WA MANISPAA WAKIONEKANA KATIKA SHUGHULI ZAO ZA UFAGIAJI BARABARA MKOANI DODOMA







 Wafanyakazi hao wanasifika sana   katika kuweka mazingira sawa mkoa huu wa dodoma hapa wanaoenekana wafanyakazi mbalimbali wakiwa katika maeneo yao ya kazi katika sehemu za mkoa huu.
Mbali na kufanya vizuri katika kuweka mzingira safi hapa manispaa ya mjini,wafanyakazi hao wailalamikia manispaa na kusema kuwa hawapewi matunzo bora katika kazi yao hiyo kwani hakuna vitendea kazi bora na wana bora vitendea kazi.Nanukuu,inafika kipindi hatuna hata buti za kuweza kuingilia kwenye  mitaro,kwani kuna uchafu mwingine unakuwa kwenye mitaro ya kupitisha maji taka tuna lazimika kuingia hivyo hivyo kutokana na ugumu wa maisha,alisikika mama mmoja ambaye alifahamika kwa jina moja mama Ester.Aliongea mama mwingine na kusema nanukuu achana na buti hata maski tu za kuzuia vumbi hatupati kwakweli tunafanya kazi katika mazingira magumu sana,hata kipato chenyewe ni kidogo sana ukiangalia na maisha ya sasa yalivyo kuwa juu tunaomba serikali kutuangalia sana sisi tunaofanya usafi wa barabarani kwani mazingira yetu sio mazuri kabisa

Picha na Habari:Paul Lawa

0 comments:

Post a Comment