BAADA YA KILIO KIREFU CHA MACHINGA COMPLEX MJINI DODOMA CHASIKIKA NA KUFANYIWA KAZI
Machinga wengi walio kuwa wakifanyia biashara zao katika eneo la oneway pamoja na majengo sasa kilio chao chasikika na kufanyiwa kazi na mkuu wa mkoa.
Nisiku chache baada ya wamachinga wengi kukimbizwakimbizwa na wagambo wa manispaa na kuswekwa rumande sasa mkuu wa mkoa wa dodoma amelipatia ufumbuzi jambo hilo na kuwasadia machinga hao.
Kulikuwa kuna maeneo mawili ambayo walitakiwa kupewa kwa ajili ya shughuli zao ndogondogo mara ya kwanza walipewa katika eneo la sabasaba ambalo kwa sasa ni eneo la soko,walikataa kutokana na kusema kuwa wenyewe ni watu wenye kipato cha chini hawawezi kuweka nyuma ya watu wenye mtaji mkubwa kwahiyo eneo hilo wakapewa wajasiliamali wengine ambao kwa sasa wanatumia kwa ajili ya soko.
Lakini mkuu wa mkoa hakusita kuendelea kuwaangalia kwa jicho la tatu mpaka alivyo ongea na utawala wa CDA na manispaa na kupata ufumbuzi wa swala hilo na kuwapatia siku chache katika eneo lililokuwa booking ya mabasi ya kusafirisha abiria scandinavia ipo karibu na round about ya kituo cha mabasi ya mkoa.
Mpaka ifikapo siku ya leo wamepewa siku ya mwisho wajenge mabanda na wasionekane tena katika maeneo ambayo sio husika kwa ajiri ya biashara ndogndogo hapa mjini.
Alisikika mwenyekiti wa wamachinga hao akisema nanukuu,yeyote atakaye kiuka amri hii kuendelea kufanya biashara katika maeneo ambayo sio husika atapigwa faini na kutopewa tena eneo la biashara.
Picha na Habari:Paul Lawa













0 comments:
Post a Comment