TOA,ACHIA,GAWA MAENEO KATIKA SOKO JIPYA LA CHADULU UGAWAJI HUO ULIO FANYWA NA MANISPAA WILAYA YA DODOMA MJINI LAZUA GUMZO NI BAADA YA WAGAIWA HAO KUTOPENDA MAENEO HAYO YA SOKO HILO
Hali ni mbaya katika soko hili kwani hakuna hata mkusanyiko wa watu hivyo basi hali inazidi kuwa mbaya kadili siku zinavyo kwenda
Na hii ni misingi ambayo ilisemekana hapa palikuwa ni viwanja vya watu lakini manispaa walivamia na kuwagaia wafanya biashara kwa muda
Hili ni banda la bwana Sadiki ambaye kwa sasa kaamia lililokuwa soko la chadulu zamani ambalo lilifahamika kama soko la mabasi mawili kama linavyo onekena pichani
kama unavyoona pichani ni baadhi ya mabanda ambayo yametelekezwa na wafanyabiashara
Takribani vibanda mia mbili havina watu wamejenga lakini cha kushangaza hakuna wakuviendeleza wengi wao wamedai kuwa hakuna mtaji wakuweza kuendeleza vibandaa hivyo kwahiyo hawawezi kwni walihaidiwa kuwa wataendelezwa kibiashara na serikali lakini kwao imekuwa tofauti,nanukuu eneo hili limevamiwa tu na serikali kwani hili eneo ni viwanja vya watu hata ukiangali utaona misingi ambayo watu wengi wameweka kwa ajili ya kuja kuendeleza maeneo yao bwana mmoja ambaye alifahamika kwa jina moja Kimalio,bwana huyo hakusita kuongea alisema tena nanukuu manispaa wamewarazimisha watu kuja kufanya biashara katika eneo hili lakini bila kuangalia mfumo mzima wa biashara inaendaje katika soko hili na kufikia wafanya biashara wenzetu kuondoka na kurudi walipo tolewa yaani wamekaidi amri ya serikali akaema kama unavyo ona mabanda mengi katika soko hili hayana watu na mpaka yana liwa na mchwa,nlizungumza na kijana mwingine ambaye alifahamika kwa jina la Elias ambaye yeye alizungumzia kuusu gharama za vibanda hivyo vinatolewaje,nanukuu unajua ndugu mwandishi haya maeneo tulipewa kwa gharama ndogo ya shilingi elfu mbili(2000)na walituambia kuwa tuyaendeleze maeneo hayo kwa kujenga mabanda ya muda mfupi na si vinginevyo haija ishia hapo walisema tutakuwa tunatoa ushuru wa shilingi mia mbili kila siku na walisema hata kama mtu haja uza wenyewe wanahitaji ushuru huo ni kwa ajiri ya kuendeleza soko.nilifanya juhudi za kumtafuta mwenyekiti wa soko hilo lakini juhudi zangu ziligonga mwamba baada ya kumkosa mtu huyo hata kwa mawasiliano hakuwa hewani hivyo basi nikajaribu kumtafuta katibu juhudi zangu ziligonga mwamba pia najitahidi niweze kumpata mwenyekiti wa soko ikishindikana kabisa ina nibidi niwatafute viongozi walio gawa maeneo nikimaanisha manispaa wenyewe
Habari na Matukio:Paul Lawa











0 comments:
Post a Comment