Saturday, August 11, 2012

Habari na Matukio

BALAA LALINDIMA KATI YA WAFANYABIASHARA WADOGOWADOGO NA MANISPAA KATIKA ENEO LA MABASI MAWILI MTAA WA CHADULU MJINI DODOMA

Kama inavyo onekana picha ni biashara ambazo zinaendelea kuuzwa katika eneo ambalo sio rasmi kwa biashara katika mtaa wa mabasi mawili mtaa wa chadulu na hawa ni baadhi ya wa mama ambao wamekiuka kauri ya manispaa ya kuama katika eneo hili
Kama unavyo ona ndugu msomaji wafanya biashara ndogondogo ambao wanafanya biashara zao katika mazingira magumu baada ya wenyewe kujitakia kwani manispaa imewapa maeneo na hawa taki kufanyia biashara katika eneo hilo
Huyu ni mama na mwanaye ambao wameka biashara zao katika eneo hilo ambalo sio rasmi na kujikuta katika asilimia kubwa wakiweka bidhaa zao chini

Baadhi ya watu ambao wanauza vyombo na wengine wakiwa wanapika viazi utamu katika eneo hilo la lililokuwa soko la mabasi mawili mtaa wa chadulu kama unavyo ona na kuna viazi utamu pembeni anaye onekana kwenye mti hapo kakaa ni muuzaji wa viazi utamu
Hapa ni mama ambaye ameweka biashara yake katika pagale moja hapa mabasi mawili yote kwa yote anajaribu kujitafutia riziki katika eneo ambalo haja ruhusiwa na serikali



Pichani ni wa mama ambao wanauza mboga aina ya sukuma wiki katika eneo hilo la mabasi mawili ambao na wenyewe wana uzia chini mboga hizo bila kujua kwamba wana weza kuleta magonjwa ya mlipuko




           Balaa lazuka ni baada ya wafanyabiashara ndogondogo lililokuwa soko la mabasi mawili mtaa wa chadulu,ni baada ya kuvunjiwa vibanda vyao na kuamishiwa katika eneo ambalo limetengwa na manispaa kwa ajili ya wafanyabiashara hao,baada ya kuamishwa wafanyabiashara hao wakiuka kauri ya manispaa na kulejea katika eneo walilokuwa mwanzo na kuacha eneo walilokuwa wametengewa na manispaa kuviacha wazi kwa muda wote na kuliwa na mchwa.
            Wafanyabiashara hao waonekana wakifanya biashara zao katika mazingira magumu sana wakionekana katika picha hapo juu ni hali halisi ya lililokuwa soko la mabasi mawili kabla ya kubadilishwa na kupewa eneo husika,wafanyabiashara hao wadai kuwa walipopelekwa na manispaa hakuna muinuko wa biashara.
             Wadai kuwa walivyo kuwa mabasi mawili walikuwa wakimaliza bidhaa zao na walivyo pelekwa soko kuu la chadulu hata mboga walikuwa hawa malizi na kauli zote hizo manispaa waonekana kukaza uzi na kutaka wafanya biashara hao wote kuamia katika soko walilopangiwa kwani pale mabasi mawili sio eneo husika kwa kufanyia biashara. 
            Baadhi ya wafanya biashara hao wamedai kuwa manispaa wanawaonea kwani wanawadai ushuru hata kama hawajauza katika eneo hilo walipo wapeleka,na wengi wao walidai kuwa katika eneo hilo waliko pelekwa hawafanyi biashara kwani wao ni wageni hivyo basi hawaja zoeleka katika eneo hilo,

Habari na Matukio:Paul Lawa

0 comments:

Post a Comment