J.K
AZINDUA AWAMU YA TATU YA TASAF KWENYE
UWANJA WA JAMHURI MJINI DODOMA.
AWAMU
YA TATU YA TASAF INAJIPAMBANUA KAMA “MPANGO WA TAIFA WA KUNUSURU KAYA MASKINI
ZILIZO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI”
HABARI
KATIKA PICHA
Umati wa Wananchi wa
Manispaa ya Dodoma waliojitokeza kwenye uzinduzi wa awamu ya tatu ya Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii – TASAF leo hii.
Rais Kikwete akiwasili
uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma maalumu kuzindua awamu ya tatu ya Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii – TASAF.
Rais Kikwete akiambatana na
viongozi wengine kwenda kuangalia Maonesho ya shughuli za wajasiriamali wadogo
waliowezeshwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF yaliokwenda sambamba na uzinduzi wa awamu ya
tatu ya TASAF.
Rais Kikwete akikagua mradi
wa upandaji miti ya matunda na vivuli wa kikundi cha wazee cha Chiwene cha
Manispaa ya Dodoma wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu ya tatu ya Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii – TASAF.
Rais Kikwete akiangalia bidhaa
zinazotengenezwa na wajasiriamali wa kikundi cha Tuamke cha Ilala Dar es salaam
kinachojihusisha na utengenezaji wa chaki na sabuni za maji wakati wa sherehe
za uzinduzi wa awamu ya tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF Mjini
Dodoma
Rais Kikwete akikagua mradi
wa ufugaji kuku chotara wa kikundi cha wajane cha Mamira Babati kilichowezeshwa
na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF wakati
wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF Mjini Dodoma
Rais Kikwete akikagua nguo
zilizoshonwa na kikundi cha Wazee cha Juhudi kutoka Manyara kilichowezeshwa na Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii – TASAF wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya TASAF
Mjini Dodoma
Habari na Dodoma Fm 98.4
Habari na Dodoma Fm 98.4








0 comments:
Post a Comment