TAFADHALI NAOMBA UPOKEE NA MTUSAIDIE KUTANGAZA:
TAARIFA MUHIMU JUU YA ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAZI
– 2012 KWA WAMILIKI WA KLABU ZA USIKU, KUMBI/SEHEMU ZA STAREHE NA WAMILIKI WA NYUMBA
ZA KULALA WAGENI
(angalia attachment)
MUHIMU:
KESHO (J.MOSI TAR. 25 AGOSTI, 2012) ASUBUHI SAA 2:30 MKUU WA MKOA
ANATAKA KUKUTANA NA RADIO ZILIZOPO KATIKA MKOA WA DODOMA KUTOA TAMKO
KUHUSU SENSA, TAFADHALI TUNAOMBA MWAKILISHI KWA AJILI YA KUJA KUREKODI.
TAARIFA
YA ZOEZI LA SENSA MKOA WA DODOMA KWA SIKU YA KWANZA (26/08/2012) KUFIKIA SAA 9
:00 ALASIRI
Zoezi la Sensa ya watu na
Makazi lililoanza usiku wa Tarehe 25 Agosti, 2012 kuamkia tarehe 26 Agosti
limeanza na linaendelea vizuri kwenye Mkoa wa Dodoma na Wilaya zake.
Akitoa taarifa za awali
jinsi zoezi la sense lilivyokwenda kuanzai usiku wa Tarehe 25 kuamkia tarehe 26
Agosti, Mratibu wa Sensa Mkoa wa Dodoma Bw. Idd Muruke amesema kuwa usiku wa
tarehe 25 makarani walianza kwa kuhesabu watu wasio na makazi maalum, watun
waliolala kwenye nyumba za kulala wageni na kwenye vituo vya usafiri kwa wale
waliokuwa safarini.
Bw Muruke anasema kwa
makundi yote waliyopanga kuyahesabu usiku huo walifanikiwa kwa asilimia mia
moja na yote walipata ushirikiano wa kutosha. Kwa siku ya leo tarehe 26 Agosti
2012 zoezi limeanza kuhesabu wanakaya kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa
Dodoma ambako nako kazi imekwenda kwa mafanikio, hajapata taarifa zozote za
changamoto zilizokwamisha kazi kutoka kwa makarani na wasimamizi wao maeneo
mbalimbali ya Mkoa na wilaya zake.
Kwa upande wa Vifaa, Bw.
Muruke amesema kuwa kufikia jana vifaa vyote muhimu kwa ajili ya kufanyia kazi
ya sensa vilikuwa vimeisha wasili na kusambazwa maeneo husika. Bw. Muruke
ameongeza kuwa wananchi wanaonekana wamehamasika kwa kiasi kikubwa na
uthibitisho unaonekana kwa jinsi walivyo na mwamko mkubwa wa kuhesabiwa na
ushirikiano mkubwa wanaowapa makarani.
Taarifa kutoka kwa
wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya zinaonesha zoezi linakwwenda vizuri.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma anasema hotuba ya jana ya Mhe Rais Kikwete,
Uhamasishaji wa wadau mbalimbali wakiwamo vyombo vya habari na vyombo vya
ulinzi na usalama vimechangia kiasi kikubwa watu kuhamasika na kushiriki
kikamilifu.
Kwa upande wa taarifa kutoka
mitaa mbalimbali ya makazi ya watu hali ni shwari, zoezi linakwenda vizuri.
Akizungumza kwenye mtaa wa Nduka Kata ya Chamwino Manispaa ya Dodoma Karani wa
Eneo hilo Bi. Julieth Paschal amesema viongozi wa mitaa na vitongoji wanawapa
ushirikiano mkubwa, wananchi wanamwamko wa kutosha na wamepata ushirikiano
mzuri kwa watu waliowahesabu kufikia mda huu japokuwa kwenye baadhi ya nyumba
hawajakuta wakazi wala taarifa kuachwa jambo linalowafanya warudi tena baadae
kuchukua taarifa kwa nyumba hizo ambazo hawakukamilisha kuchukua taarifa.
Kwa upande wa wananchi
waliohesabiwa wameonesha kuwa zoezi la sensa ni jambo la kawaida na wameridhika
nalo, akizungumza kama alivyokutwa kwenye kaya yake mtaa wa Nduka Kata ya
Chamwino Manispaa ya Dodoma Bw. Nazareth Mwenda amesema kuwa taifa linakabiliwa
na changamoto nyingi kama ukosefu wa ajira kwa vijana, watoto wa Mtaani hivyo
serikali inahitaji kuwa na takwimu sahihi kupitia zoezi la Sensa ili iweze
kupanga bajeti yake inayozingatia mipango sahihi ya maendeleo inayozingatia
changamoto hizo na amewataka wananchi wote kwa vigezo hivyo alivyotoa washiriki
kikamilifu kuhesabiwazoezi la sensa

0 comments:
Post a Comment